Afya bora kupitia utafiti!

Utafiti wa Vijana wa Mombasa ('Mombasa Youth Study’) inasajili vijana wa Mombasa ili watueleze ilivyo kuishi hapa, na jinsi tunaweza kuboresha huduma za afya. 

Washiriki wanaombwa kukamilisha utafiti mfupi, ambao unapaswa kuchukua dakika 5-15 kukamilika. Unaweza kuukamilisha kwa Kiingereza au Kiswahili. Majibu yako yatasaidia kuunda huduma za afya na kuongoza utetezi katika  kanda. Ukishiriki katika utafiti huu, utakuwa unasaidia kuboresha huduma za afya kwako na kwa jamuii yako. 

Data yoyote unayoshiriki itashughulikiwa kwa usiri wa hali ya juu. Haitashirikiwa kamwe na mtu yeyote nje ya timu ya utafiti, wakiwemo wazazi na walimu wako.

Tafadhali pitia kila moja ya kauli zifuatazo:

  • Nimesoma fomu ya maelezo ya utafiti

  • Nilipokuwa na maswali yoyote, niliwasiliana na timu ya watafiti (kupitia kwa nambari (via +254 113 280 528 or info@mombasayouthstudy.com)  na kujibiwa.

  • Ninaelewa kuwa ninaweza kuondoa idhini yangu wakati wowote kwa kufunga tu dirisha la utafiti. 

  • Ninaelewa kuwa kukamilisha utafiti huu si sharti la kuajiriwa kwangu, wala majibu yangu hayatashirikiwa na mwajiri wangu. 

  • Ninaelewa kuwa nikiondoa idhini yangu, hii haitaathiri uhusiano wangu na Médecins Sans Frontières au Idara ya Afya ya Kaunti ya Mombasa. 

  • Ninaelewa kuwa taarifa zozote ambazo nitachangia katika utafiti huu zitashughulikiwa kwa usiri na kupatikana tu na wafanyakazi walioidhinishwa wa utafiti.